Siku ya tatu ya sikukuu ya Idul-Adh-ha… Atabatu Abbasiyya bado inaendelea kupokea wageni

Maoni katika picha
Siku ya tatu mfululizo katika siku za Idul-Adh-ha idara za Atabatu Abbasiyya tukufu zinaendelea kupokea mazuwaru kutoka ndani na nje ya Karbala, kutokana na mazingira mazuri yaliyopo katika eneo hili takatifu la malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) yaliyojaa marashi ya imani.

Ziara wanazofanya ni sehemu ya burudisho la nafsi kwao na sehemu ya furaha, wanajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na kuomba shifaa (uombezi) kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), sikukuu hii ni nafasi kwao ya kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu.

Katika mazingira hayo ya kiimani, Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kila iwezalo kuhakikisha mazingira yanakua ya amani na tulivu, watumishi wa vitengo vyote wamejipanga kuwatumikia mazuwaru na kuhakikisha wanafanya ziara kwa utulivu, kuna usimamizi maalum katika siku hizi, nao ni muendelezo wa utaratibu uliowekwa usiku wa Arafa na mchana wake, vitengo vyote vinahakikisha kuna amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: