Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu inafanya semina ya usomaji sahihi wa Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya semina ya Qur’ani katika mji wa Kufa, wanasomesha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu.

Kiongozi wa idara ya usomaji Sayyid Ahmadi Zamiliy amesema: “Semina hii inalenga kuibua vipaji vya usomaji wa Qur’ani na kuhifadhi”, akahimiza “Ulazima wa kuandaa kizazi cha wasomi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu watakao kuwa mbegu bora ya kusambaza elimu ya Qur’ani katika jamii”.

Akaongeza kuwa: “Semina itadumu kwa muda wa wiki sita, kila wiki itakua na mihadhara mitano chini ya msomaji Ahadi Abduzuhura, semina inawashiriki zaidi ya 25 wenye umri kati ya miaka 10 hadi 16”, akafafanua kuwa: “Semina inafanywa kwa kusirikiana na msikiti wa Imamu Albaaqir (a.s) katika mji wa Kufa”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu, husimamia harakati nyingi zinazo husu Qur’ani tukufu na miradi mbalimbali, kwa wanafunzi na walimu wa vyuo vikuu na hauza wakati wote wa mwaka, pamoja na semina za Qur’ani za majira ya joto, kupitia semina hizo mamia ya washiriki wamehitimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: