Kitengo cha malezi na elimu ya juu kinajadiliana na taasisi ya Ain njia za kushirikiana na kubadilishana uzowefu

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, umetembelea taasisi ya Ain katika mji mkuu wa Bagdad, na kukagua vituo vya (Nyota zing’aazo) vilivyo chini ya taasisi hiyo, vituo maalum vya kulea mayatima kutoka mikoa tofauti.

Ziara inalenga kuangalia njia za kushirikiana kati ya kitengo cha malezi na elimu ya juu na taasisi za kijamii zinazofanya kazi chini ya mwamvuli wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, ikiwemo taasisi ya Ain.

Ziara hii pia inalenga kuangalia uzowefu wa taasisi katika kushughulikia matatizo ya watoto, kwa kuanzisha vituo maalum kwenye sekta za malezi katika (vituo vya nyota zing’aazo), ikiwa ni pamoja na kubaini na kutoa tiba za kinafsi.

Pande mbili hizo zimejadili njia za kushirikiana na kubadilishana uzowefu na uwezekano wa kitengo cha malezi na elimu ya juu kusaidia taasisi ya Ain, Ziara hii itafuatiwa na ziara zingine sambamba na warsha ili kufikia viwango vya juu kabisa vya utoaji wa huduma bora.

Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu kinaimarisha mawasiliano na ushirikiano na taasisi za kiraia zinazotoa huduma za kibinaadamu, zikiwemo taasisi zinazolea mayatima.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: