Kufanikiwa kwa ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika ziara ya Arafa na Idul-Adh-ha

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa ulinzi, utoaji wa huduma, afya na ratiba maalum katika ziara ya usiku wa Arafa, mchana wake na siku tukufu za Idul-Adh-ha.

Mkakati huo umetekelezwa na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye sekta ya ulinzi, utoaji wa huduma na afya, maandalizi yalikamilika siku chache kabla ya siku ya Arafa, kwani tulitarajia kuwa na idadi kubwa ya mazuwaru, hususan baada ya kusimama ziara hiyo kwa zaidi ya miaka miwili, kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya Korona, huduma zilizotolewa zinaendana na wingi wa mazuwaru waliomiminika kwa muda wa zaidi ya siku tano.

Utoaji wa huduma maalum ulianza asubuhi ya siku ya Arafa hadi usiku wa Idul-Adh-ha na mchana wake na kuendelea katika siku zote za sikukuu, watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na wasaidizi wa kujitolea wamefanya kazi kubwa, ziara imefanywa kwa utaratibu mzuri bila kutokea msongamano wowote pamoja na idadi kubwa ya watu waliokuja kufanya ziara.

Vitengo vingine pia vimepata mafanikio makubwa katika shughuli zao, kama vile kitengo cha (Dini, Tablighi, Qur’ani, Utamaduni na Habari) na sekta zingine.

Kumbuka kuwa kukamilika kwa ziara hii ni mwanzo wa maandalizi ya kupokea sikukuu kubwa ya Idul-Ghadiir, sikukuu hiyo imeandaliwa ratiba maalum inayo endana na utukufu wa siku hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: