Kutandikwa mazulia mapya kwenye ukumbi wa wanawake katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f)

Maoni katika picha
Watumishi wa Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamemaliza kutandika mazulia mapya sahemu iliyokua imebaki ndani ya ukumbi wa wanawake.

Rais wa kitengo hicho Adnani Dhaifu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kutandika mazulia mapya sehemu ya wanaume, tulianza kutandika na sehemu ya wanawake baada ya kuwasili mazulia maalum ya kutandikwa sehemu hiyo, nayo ni miongoni mwa aina za kifahari”.

Akaongeza kuwa: “Eneo lote lililotandikwa limefika mita za mraba (400) kwa kumbi zote mbili, kazi ya kutandika ilianza baada ya kuondoa mazulia ya zamani na kuyapeleka kuoshwa, tulianza kwa kupiga deki na kusafisha ukuta kisha ndio tukatandika mazulia mapya”.

Akabainisha kuwa: “Mazulia yamegawanya kwa kufuata vipimo, nayo ni miongoni mwa aina za kifahari na yanaubora mkubwa, rangi yake inafanana na mazulia yaliyotandikwa kwenye ukumbi wa wanaume, hivi sasa kumbi zote zinamuonekano mzuri na zinakaribisha mazuwaru wanaokuja kufanya ibada jirani na Imamu wao msubiriwa (a.f)”.

Kumbuka kuwa Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) ni miongoni mwa Maqaam muhimu sana katika mji wa Karbala, kutokana na kufungamana kwake na Imamu Mahadi (a.f), mazuwaru wengi huelekea hapo baada ya kufanya ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: