Kuendelea kwa shughuli za mradi wa (Ainul-Hayaat) kwa wanafunzi wa kike

Maoni katika picha
Kitengo cha masomo ya Qur’ani katika chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) cha wasichana, chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinaendelea na shughuli za mradi wa (Ainul-Hayaat).

Rais wa chuo Shekhe Hussein Turabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huu ni mradi wa kielimu unahusisha mashindano ya kitafiti kuhusu fani za Qur’ani tukufu na tafsiri yake, Fiqhi, Aqida, Historia ya Mtume na Maasumina (watakasifu), wanachuoni wa madhehebu ya Imamiyya na vitavu vyao, na vinara wa wanawake wa kishia”.

Akaongeza kuwa: “Tunafanya mradi huu kwa ajili ya kuongeza kiwango cha elimu ya wanafunzi wetu, kwa kuwafundisha masomo tofauti na kuwapa majaribio, mradi huu unamchango mkubwa sana wa kuongeza elimu kwa wanafunzi”.

Akasema: “Hakika mradi unajenga ushindani kwa wanafunzi, kunazawadi maalum zimeandaliwa kwa washindi mwishoni mwa mradi, mshindi wa kwanza atazawadiwa kwenda kumzuru Imamu Ridhwa (a.s) na mshindi wa pili kwenda kumzuru bibi Zainabu (a.s), mshindi wa tatu atapewa kompyuta mpakato (labtot), mshindi wa nne na wa tano watapewa simu”.

Akabainisha kuwa: “Baada ya kumaliza mashindano yote wale waliopata alama za juu wataingizwa kwenye hatua ya kupigiwa kura mwaka 2023m”.

Tambua kuwa: “Mradi huu ni kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu tu, mitihani itatolewa kwa njia ya mtandao wa Ummul-Banina (a.s) kupitia program ya Siraji, kila mtihani utakua na maswali (20) kulingana na somo husika”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: