Wasimamizi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa wanaendelea kuhuisha maadhimisho ya kujenga uwezo wa kiroho kwa washiriki.
Katika usiku wa Ijumaa wamesoma Dua Komail bun Ziyaad (a.s) na Ziaratu-Ashuraa na Ijumaa Asubuhi wakasoma Dua Nudba, kumkumbuka Imamu wa zama (a.f).
Kumbuka kuwa mradi huu ni sehemu ya ratiba ya kuboresha usomaji wa Qur’ani kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18, na hii ni awamu ya sita kufanywa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.