Wanafunzi wa vyuo vikuu wanatembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule, kimeratibu ziara ya wanafunzi wa vyuo vikuu ya kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pembezoni mwa ushiriki wao kwenye hafla ya wahitimu wa vyuo.

Kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo na shule Sayyid Maahir Khalidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ratiba ya halfa ya wanachuo inavipengele vingi, miongoni mwake ni kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Wametembelea (shirika la teknolojia ya kilimo na viwanda Khairul-Juud – Darul-Kafeel ya uchapaji na usambazaji – kiwanda cha maji ya Alkafeel), wakati wa ziara wamepewa maelezo ya utendaji wa miradi hiyo na teknolojia zinazo tumika kwa kila mradi”.

Mwisho wa ziara wanafunzi wameshukuru sana wasimamizi wa program hii na Atabatu Abbasiyya kwa ujumla, kwa kuwapa nafasi ya kutembelea miradi hiyo, wakaomba ziara kama hii itokee tena siku za zijazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: