Mwisho wa hafla ya wahitimu wa vyuo vikuu iliyoandaliwa na Atabatu Abbasiyya jioni ya Jumamosi, kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesema.
Mimi nahisi majukumu katika nafsi yangu, kabla yenu tulifanya hafla ya wahitimu mahala hapa, daima tupo tayali kuwahudumia na tunamuomba Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi mambo yenu.
Tunatamani wakati wote alitunuku amani taifa letu kwa uwepo wenu, nina hofu pia, mnajua hufu hutokea katika jambo linaloweza kutokea au lisitokee, hofu sio huzuni, kwani huzuni hutokea katika jambo lililofanyika na hofu kwa jambo lijalo.
Ninahofu nyuso hizi nzuri zisijekuhama na kwenda nje ya nchi, taifa hili linahaki kwetu wote, yatupasa tuvumilie na tufanye kazi ya kubadilisha mazingira, natoa wito kwa kila mtu awajali wahitimu na kuwatengenezea fursa za kufanya kazi.
Iraq haijengwi ispokua na wairaq wenyewe, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Iraq itaimarika kwenye sekta zote, elimu, afya, uchumi, na utawala chini ya utendaji wenu.
Nawaombea mafanikio mema nyie na wale ambao hawakupata nafasi ya kuwapamoja na sisi hapa bila kusahau wazazi wetu watukufu, hakika kuwafanyia wema wazazi ndio neema, mafanikio ya mwanaadamu hupatikana kwa kumfanyia wema mama na baba.
Elimu ni amana kwenu na ukarimu huu pia ni amana tunawatarajia mje kutumikia taifa na raia wake, namuomba Mwenyezi Mungu akuwezesheni na ninawashukuru.