Kupandishwa kwa bendera ya Ghadiir katika haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Ukumbi mtukufu wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) jioni ya Jumapili imefanywa shughuli ya kupandisha bendera ya Idul-Ghadiir itakayo adhimishwa kesho tarehe kumi na nane Dhulhijja, bendera imepandishwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini mbele ya baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo, watumishi na mazuwaru, wote walisimama pembeni ya jukwaa ilipopandishwa bendera hiyo.

Tukio hilo lilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Badri Mamitha kutoka idara ya Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya, ukafuata ujumbe uliotolewa na msaidizi wa makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya bwana Ali Saffaar, akaongea kuhusu ukubwa wa tukio la Ghadiir, kwalo Dini ilikamilika na neema ikatimia kwa kutazwa kiongozi wa waumini Ali (a.s), sambamba na kusoma kaswida inayo endana na tukio hilo.

Kisha katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu akapandisha bendera iliyoandikwa hadithi ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Niliyekua kiongozi wake basi huyu Ali ni kiongozi wake), huku sauti za furaha ya Ghadiir na dua zikisikika kufurahia kukamilika Dini na kutimia kwa neema, Idul-Ghadiir Aghar.

Tambua kuwa bendera hiyo ilitolewa zawadi na Atabatu Alawiyya tukufu kwa ajili ya kupandishwa leo siku tukufu, kama alama ya kuanza kwa furaha za Ghadiir chini ya uratibu wa Atabatu Abbasiyya takatifu.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya imesha andaa utaratibu maalum wa kuadhimisha siku hiyo utakaodumu siku kadhaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: