Masayyid wanaotoa huduma Ataba wanapokea mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa maneno mazuri na mauwa

Maoni katika picha
Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanapokea mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa maneno mazuri na kugawa pipi katika kumbukumbu ya Idul-Ghadiir, siku aliyotawazwa babu yao Ali bun Abu Twalib (a.s) na Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu kuwa khalifa, wasii, Imamu na kiongozi baada yake.

Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu leo Jumatatu wamesimama kwenye milango ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakikaribisha mazuwaru na kugawa pipi kwa watu wanaokuja kumzuru bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika siku hii ambayo ilikamilika Dini na kutimia neema.

Tambua kuwa ni kawaida ya Masayyid wanaotua huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu kufanya hivyo kila mwaka, wanaonyesha namna wanavyo wapenda na kushikamana na Ahlulbait (a.s), na namna wanavyo fungamana nao kiroho na kufuata mwenendo wao mtukufu, hakika wao ndio njia iliyo nyooka tuliyoambiwa na Mtume (s.a.w.w), jambo hilo huleta furaha kwa mazuwaru na huwajenga katika kushikamana na wilaya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: