Zapazwa sauti za washairi baina ya haram mbili za watoto wa aliyepewa kiapo cha utii Ghadiir

Maoni katika picha
Uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu ya Imamu Hussein na ngugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), imefanywa hafla ya kuadhimisha Idul-Ghadiir, siku ambayo Imamu Ali (a.s) alitangazwa rasmi kuwa kiongozi wa waumini na khalifa wa waislamu, Mtume (s.a.w.w) akashushiwa aya ya ufikishaji (Tablighi) kutokana na umuhimu wake.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Muhammad Ridhwa Swaraaf, na kuhudhuriwa na watu wengi, wakiwemo mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mazingira yaliyojaa shangwe na furaha.

Hafla hilyo imehudhuriwa pia na kundi la waimbaji na washairi wa Imamu Hussein, miongoni mwao ni muimbaji Hussein Abu Shairi Karbalai, Farasi Asadiy Karbalai, Hussein Swabahi Karbalai, Haidari Mwalimu Karbalai na Hussein Akili Karbalai.

Wameimba kaswida na mashairi ya kuonyesha mapenzi kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) na watoto wake Maimamu watakasifu (a.s), pamoja na mapenzi ya Iraq sambamba na vionjo murua vya uimbaji ambavyo ni mara chache kusikika, huku hafla yote ikijaa shangwe na furaha.

Hafla imepambwa na maneno matamu kutoka kwa muongozaji wa hafla Hassan Najaari kwa kuongea semi mbalimbali zinazofungamana na dua za kuomba amani na utulivu katika mji wa Imamu Ali (a.s) na maeneo yanayo uzunguka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: