Idul-Ghadiir ni sikukuu tukufu.. mada ya mhadhara wa kidini ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kimeandaa mihadhara ya Dini katika kuadhimisha Idul-Ghadiir asubuhi ya Jumatatu, ndani ya uwanja wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na kundi la mazuwaru wa malalo hiyo takatifu.

Mzungumzaji alikua ni Shekhe Muhammad Kuraitwi kutoka kitengo cha Dini, ameongea kuhusu maadhimisho hayo, amefafanua kuwa siku hiyo ni sikukuu kubwa, kwani ni siku ya kukamilika Dini na kutimia neema, hakuna neema kubwa zaidi ya kukamilika Dini, neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, akasisitiza kuwa neema hii inastahiki kushukuriwa.

Akaongea pia kuhusu ukubwa wa maadhimisho haya na athari yake katika Dini ya kiislamu, akaeleza umuhimu wa kusherehekea Idul-Ghadiir na kuhuisha utiifu kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).

Akataja utukufu wake na akasema kuwa kusherehekea Idul-Ghadiir ni kuadhimisha alama kubwa ya Uislamu, Qur’ani imethibitisha umuhimu wake kama inavyosema katika aya ya Tablighi, hakika kufurahi na kusherehekea siku hii ni miongoni mwa Tablighi, kuhuisha siku hii kunawaonyesha watu maudhui ya Uimamu.

Shekhe Kuraitwi akataja hadithi nyingi za Mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s), zinazo eleza umuhimu wa tukio hilo na kusisitiza kuwa hiyo ndio sikukuu kubwa katika Uislamu, nayo ni siku aliyotangazwa Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) kuwa kiongozi wa waislamu, watu walijulishwa pia ni usia wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: