Madrasa ya kuandaa kizazi cha wasomi wa Qur’ani imesema.. Zaidi ya wanafunzi 6000 wameshiriki kwenye semina za Qur’ani katika mji wa Najafu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa wanafunzi (6363) wameshiriki kwenye semina za Qur’ani za majira ya joto.

Mkuu wa Maahadi Sayyid Muhandi Almayali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mradi wa semina za Qur’ani za majira ya joto mwaka huu umepata muitikio mkubwa, miongoni mwa mikoa iliyopata washiriki wengi ni mkoa wa Najafu, tumewagawa kwenye vituo sita ambavyo ni: (Makao mkuu ya mkoa – Kufa – Abbasiyya – Almashkhaab – Mtaa wa Alhuriyya – Mtaa wa Radhawiyya), kila kituo kimekua na vikao vingi vya usomaji wa Qur’ani chini ya usimamizi wa wabobezi”.

Akaongeza kuwa: “Selebasi inayotumika kwenye semina hizi ni ileile inayotumika kwenye semina zinazofanywa na Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, sambamba na kuhuisha matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s)”.

Akafafanua kuwa: “Idara ya Maahadi inafuatilia kwa karibu semina zote, kwa kutuma watu kwenye vikao vya usomaji, ambao huhoji washiriki na wakufunzi sambamba na kuzungumza maneno ya kushajihisha wanafunzi na kuwapa mbinu za ufundishaji wenye mafanikio wakufunzi”.

Tambua kuwa wilaya ya Najafu inawashiriki (1363), na Kufa Zaidi ya wanafunzi (500), mtaa wa Harbiyya Zaidi ya wanafunzi (1500), na Mashkhabu wanafunzi (500), Abbasiyya wanafunzi (1500) na mtaa wa Raudhiyya wanafunzi (1000).

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu imefanya semina za Qur’ani katika majira ya joto, miongoni mwa masomo yaliyofundishwa ni lugha, aqida, akhlaqi, sira na Qur’ani tukufu, jumla wa wanafunzi elfu kumi na tatu wameshiriki kwenye semina hizo kutoka mkoa wa Najafu, Waasitu, Misaan na Diwaniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: