Kuanza kwa semina inayohusu usanifu wa picha (Graphic Design)

Maoni katika picha
Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya semina yenye anuani isemayo (Misingi ya Graphic Design) kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na wajumbe wa Skaut ya Alkafeel.

Mkufunzi wa semina hiyo bwana Ali Salim amesema: “Semina inalenga kuwatambulisha washiriki misingi ya Program za (Photoshop) na namna za kuzitumia katika usanifu na utengenezaji wa picha”.

Akaongeza kuwa: “Semina ilikua na vipengele vingi, miongoni mwake ni: Maana ya kudizain, Program za kudizain, utengenezaji wa picha, vifaa vya kufanyia dizain, vifaa vya kuchorea”. Akasema: “Semina imedumu kwa muda wa siku (5) muda wa masomo ulikua saa (3) kila siku”.

Kumbuka kuwa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea kuratibu warsha na semina za kielimu kwa lengo la kukuza uwezo wa watumishi wa Ataba kwenye mambo mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: