Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanza program ya kutoa mafunzo ya kujenga uwezo wa watumishi wa kitengo cha malezi na elimu wanaofanya kazi katika shule za Al-Ameed.
Makamo kiongozi mkuu wa kitengo cha malezi Dokta Hassan Daakhil amesema: “Ratiba ya masomo haya inalenga kujenga uwezo wa watumishi”.
Akaongeza kuwa: “Ratiba hii inahusisha watumishi wote wa idara ya malezi na elimu”.
Akasisitiza kuwa: “Lengo kuu la program hii ni kuboresha uwezo wa watumishi sambamba na kujenga uaminifu kwa jamii”.
Tambua kuwa program inafanyika sambamba na uboreshaji wa sekta ya malezi na elimu, kwa kuandaa watumishi waliobobea kwenye mambo yote, watakao weza kutoa malezi bora yenye tija.