Atabatu Abbasiyya yasisitiza kuwa ipotayali kusaidia ujengaji wa fikra za kibinaadamu na sekta ya elimu

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umesisitiza umuhimu wa kujenga fikra za kibinaadamu na sekta ya elimu kwa hali na mali, hayo yamesemwa katika ujumbe uliotolewa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Sayyid Ali Swafaar makamo katibu mkuu, katika hafla ya kuwapongeza washindi wa shindano la maarifa ya turathi za vikundi katika mwezi wa Ramadhani.

Makamo katibu mkuu Sayyid Ali Swafaar amesema: “Atabatu Abbasiyya tukufu inasimama pamoja na taasisi za sekula na utamaduni kutokana na umuhimu wa elimu, na nafasi yake katika kujenga jamii ya wanaadamu wastarabu, na kuboresha maadili ya watu”, akaongeza kuwa: “Msaada wa Atabatu Abbasiyya katika sekta ya elimu unalenga kuimarisha taasisi za kielimu sambamba na kufungua vituo vya bobezi mbalimbali za kielimu”.

Akabainisha kuwa: “Kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) na usimamizi wa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, tumepata mafanikio makubwa kwenye sekta ya elimu na sekta ya turathi za kiislamu”. Akaendelea kusema: “Atabatu Abbasiyya tukufu inajali sata tabaka la vijana, hususan vijana waliopo vyuoni, Ataba imeunda idara maalum kwa ajili ya kusaidia watu hao muhimu kupitia program tofauti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: