Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla kubwa ya kusherehekea Idul-Ghadiir katika bustani za Alkafeel na kuhudhuriwa na kundi kubwa la familia za Karbala, zilizokuja kuhuisha utiifu kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s).
Hafla hiyo imefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na kundi la washiriki wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, unaosimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Baaba ya ufunguzi huo masikio ya wahudhuriaji yakaburudishwa kwa sauti nyororo za mashairi yaliyosomwa na (Zainul-Aabidina Saidi – Farasi Asadi – Ali Abdulhussein Anmbari – Mauhubu Muhammad Baaqir Qahtwani – Muhammad Amiir Tamimi).
Mashairi yao yalijaa sifa za bwana wa mawasii Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), na kuhuisha tukio kubwa katika historia ya mwanaadamu, wakaeleza mtazamo wa kiimani na kidini kuhusu Ghadiir.
Tambua kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuadhimisha kumbukumbu hiyo tukufu, yenye vipengele vingi na itakayo dumu kwa muda wa siku kadhaa, miongoni mwa vipengele vya ratiba hiyo ni hafla hii.