Kuanza kwa kongamano la kielimu na kimataifa awamu ya kwanza kuhusu Answaru wa Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Shughuli za kongamano la kwanza la kielimu na kimataifa kwa Aswaru wa Imamu Hussein (a.s) zimeanza asubuhi ya Alkhamisi chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).

Kongamano linasimamiwa na jumuiyya ya Al-Ameed na chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kauli mbiu isemayo: (Sitambui wafuasi waaminifu na bora kushinda wafuasi wangu), na anuani isemayo (Answaru wa Imamu Hussein “a.s” ni msingi wa uhai), litadumu kwa muda wa siku mbili.

Shughuli za ufunguzi zimehudhuriwa na wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu na viongozi wengine, bila kusahau wawakilishi wa sekta mbalimbali kutoka ndani na nje ya Iraq.

Baada ya Qur’ani ya ufunguzi iliyosomwa na Sayyid Hasanaini Halo, imesomwa surat Faat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa).

Ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi.

Kisha mshairi Ali Swafaar Karbalai akasoma kaswida. Halafu kikao rasmi cha uwasilishaji wa mada za kitafiti kikaanza chini ya usimamizi wa Dokta Sarhani Jafaat Salmani, jumla ya mihtasari ya mada tatu ikawasilishwa ambayo ni:

  • - Historia ya Abdullahi bun Afiif Azdiy, imewasilishwa na Dokta Abdulkhaliq Khamisi Ali.
  • - Swahaba Anasi bun Harithi Alkahiliy (r.a), uchambuzi wa historoa yake ulio wasilishwa na Dokta Salaam Jabaar Munshidu na mtafiti Zainabu Rahmani Muhammad Saidi.
  • - Mitazamo ya kihistoria katika khutuba za Shahidi Zuhauru bun Qain Albajaliy (r.a) siku ya Ashura, imewasilishwa na Dokta Faadhil Kaadhim Swadiq Al-Abaadi.

Tunatarajia kuendelea kwa brogram za kongamano, kutakua na kikao cha pili leo Alasiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: