Maandalizi ya mwisho ya kufanya hafla ya wahitimu wa mradi wa semina za Qur’ani za majira ya joto

Maoni katika picha
Maandalizi ya kufanya hafla ya wahitimu wa mradi wa semina za Qur’ani za majira ya joto yapo katika hatua za mwisho.

Hafla hiyo itafanywa ndani ya ukumbi wa jengo la Al-Ameed jioni ya kesho siku ya Ijumaa mwezi 22 Dhulhijja, na kushiriki maelfu ya wanafunzi walionufaika na mradi huo mkubwa wa Qur’ani tukufu hapa Iraq.

Rais wa Majmaa ya Qur’ani tukufu Dokta Mushtaqu Ali amesema: “Washiriki jumla walifika elfu 42 kwenye mradi wa semina za Qur’ani za majira ya joto kutoka mikoa tofauti ya taifa letu kipenzi, wingi huo unaonyesha wazi umuhimu wa mradi huu, uliosimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa (Karbala na Najafu) na matawi yaliyochini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, baada ya mafanikio hayo Maahadi inajiandaa kufanya hafla kubwa ya kutangaza mafanikio yaliyopatikana kwenye mradi wake uliotekelezwa kwa wiki kadhaa kwenye mikoa mingi hapa nchini”.

Maandalizi yamehusisha usafiri kutoka kitengo cha magari ya Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kubeba washiriki kutoka nje ya mkoa wa Karbala, na kuwapatia mambo yote muhimu yanayo hitajika baada ya kufika kwao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: