Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu unatoa pongezi za kumbukumbu ya Idul-Ghadiir kwa katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu Sayyid Issa Khurasani amepokea ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, uliokuja kumpongeza kufuatia kumbukumbu ya Idul-Ghadiir Aghar.

Ugeni huo umeongozwa na makamo rais wa kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Jalukhani Mussawi, wamepeana pongezi na maneno mazuri kufuatia tukio hili.

Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umepongeza shughuli zilizofanywa katika wiki ya Ghadiir Aghar, wakaomba wadumu katika taufiq ya kusimama pamoja na kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).

Naye katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya ameonyesha furaha kubwa kwa kufikiwa na ugeni huo mtukufu ambao ni kielelezo cha kuimarika mahusiano baina yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: