Jioni ya Alkhamisi Atabatu Abbasiyya tukufu imepokea miili ya mashahidi wa shambulio la bomu lililotokea katika mji wa Zakhu jana siku ya Jumatano.
Miili hiyo imepitishwa ndani ya haram ya Abbasi na kundi kubwa la waumini, imeswaliwa na kufanyiwa ibada ya ziara na masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu.