Wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, unaosimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya wanashiriki katika usomaji wa vikundi kwa mahadhi ya kiiraq na kimisri kwenye mahafali mbalimbali ndani na nje ya Ataba takatifu.
Wanafunzi hao wameshiriki kwenye ratiba ya kuwajengea uwezo watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, hafla ya kupandisha bendera ya kiongozi wa waumini (a.s) kwenye Idul-Ghadiir, iliyoandaliwa na Mawakibu za Karbala kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Hali kadhalika wameshiriki kwenye hafla ya kuhitimisha semina za majira ya joto, iliyoratibiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani, iliyofanywa ndani ya msikiti wa Kufa na kwenye hafla zingine.
Ushiriki huo ni sehemu ya ratiba ya kujenga uwezo wao.
Kumbuka kuwa mradi huo unafanywa na Atabatu Abbasiyya chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu.