Atabatu Abbasiyya tukufu jioni ya Ijumaa imefanya hafla ya kuhitimu wanafunzi wa mradi wa semina za Qur’ani za majira ya joto.
Hafla hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa jengo la Al-Ameed na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na makamo katibu mkuu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na kijana Yasini As’adi, ikafuata surat Faat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa (Lahnul-Ibaa).
Ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, uliowasilishwa na rais wa Majmaa ya Qur’ani tukufu katika Ataba Dokta Mushtaqu Ali.
Ukafuata ujumbe wa wahitimu uliowasilishwa na mwanafunzi Muhammad Mustwafa, akaishukuru Atabatu Abbasiyya hasa Majmaa ya Qur’ani tukufu kwa kuandaa mradi huo ambao wamejifunza usomaji sahihi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na kukihifadhi, sambamba na kusoma Aqida, Fiqhi, Akhlaq na historia ya Mtume na Maimamu watakasifu (a.s).
Halafu wanafunzi wanaohitimu wakasoma kaswida maalum ya mradi, aidha mwanafunzi mshairi Muhammad Baaqir Qahtwani alipata nafasi ya kusoma mashairi kwenye hafla hiyo.
Hafla ikahitimishwa kwa wanafunzi wanaohitimu kuhuisha ahadi na kusoma Dua Faraji.
Kumbuka kuwa jumla ya wanafunzi walioshiriki kwenye mradi wa semina za majira ya joto ni elfu 42 kutoka mikoa tofauti ya Iraq.