Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki kwenye mkutano wa makatibu wakuu wa Ataba za ndani na nje ya Iraq

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Aali Dhiyaau-Dini imeshiriki mkutano wa makatibu wa Ataba za ndani na nje ya Iraq, uliofanywa katika malalo ya kiongozi wa waumini Ali (a.s).

Kikao cha ufunguzi kimeongozwa na rais wa Wakfu-Shia Dokta Haidari Shimri, mbele ya wawakilishi wa Ataba tukufu za Husseiniyya, Kadhimiyya, Radhawiyya, Askariyya, Abbasiyya, Zainabiyya na mazaru tukufu za ndani na nje ya Iraq.

Rais wa Wakfu-Shia Dokta Haidari Shimri amesema: “Mkutano wa makatibu wa Ataba tukufu utawekwa kwenye orodha ya mikutano itakayo endelea kufanywa siku za mbele kwa makatibu na manaibu wao, zinaweza pia kushiriki idara tofauti za Ataba kwa lengo la kuweka ratiba ya pamoja ili kuboresha huduma kwa mazuwaru”.

Akaongeza kuwa: “Viongozi wakuu wa Ataba wanafanya kazi kwa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Sistani, jukumu lao kubwa ni kutumikia mazuwaru kwa kutoa hutuma mbalimbali pamoja na kufanya miradi ya utoaji wa huduma za kijamii na ujenzi, kuna ratiba za pamoja katika kuwajenga mazuwaru kidini na kitamaduni kwa kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.

Kumbuka kuwa mkutano huu ni msingi wa mikutano mingine ijayo, itakayo lenga kutengeneza mfumo mmoja utakao tumiwa na Ataba zote katika kuhudumia mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: