Mshiriki kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu amepata tuzo kwenye shindano la kimataifa (35 AWARDS) lililokua na washiriki 124827 kutoka nchi 174

Maoni katika picha
Mpigapicha kutoka kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya Samiri Khalili Ibrahim Alhusseiniy amepata tuzo kwenye shindano la kimataifa la (35 AWARDS) kwa kupata asilimia (100) ya upora wa picha nyeupe na nyeusi kwenye shindano la awamu ya saba, ambalo washiriki walikua (124,827) kutoka nchi (174) pamoja na Iraq.

Alhusseiniy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi niliyoshiriki ilikua na anuani isemayo (mwanamke mwenye huzuni), nayo ni moja ya picha nilizopiga katika shughuli za Atabatu Abbasiyya tukufu nje ya Iraq, kulikua na ushindani mkali, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu na baraka za ninaemtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s) nimepata ushindi huu na kuzishinda zaidi ya picha (470) kutoka nchi tofauti”.

Akabainisha kuwa: “Shindano hili lilikua na majaji (50) wa kimataifa, Picha zote wamezikagua na kuzichuja katika hatua ya kwanza, kisha picha zilizopita wanazipigia kura kuingia hatua ya pili kisha zinaingizwa hatua ya mwisho ambayo picha yangu imeibuka na ushindi pia”.

Tambua hii sio tuzo ya kwanza kuipata Husseiniy, amesha shiriki mara nyingi kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa na kupata tuzo. Huu ni muendelezo wa kuendelea kupata tuzo na msingi wa kuendelea kushiriki kwenye mashindano yajayo.

Kumbuka kuwa ushiriki wa shindano hili na kupata tuzo ni moja ya mfululizo wa tuzo wanazopata wapigapicha wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa, kutokana na uzowefu walionao na weledi wa hali ya juu, sambamba na msaada wanaopewa na viongozi wa kitengo, bila kusahau uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unaofanya kila uwezalo kuboresha uwezo wa watumishi wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: