Kutoa sadaka ya pete.. shuhuda kutoka kwa Mtume kuhusu uongozi wa kiongozi wa waumini Ali (a.s)

Maoni katika picha
Siku ya mwezi ishirini na nne Dhulhijja tunakumbuka kutoa sadaka ya pete kiongozi wa waumini (a.s) wakati anaswali, kutokana na umuhimu wa kumbukumbu hiyo na yatokanayo nayo, Mwenyezi Mungu alishusha aya isemayo: (Hakika kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao wanasimamisha swala na kutoa zaka wakiwa wamerukuu * Na mwenye kumtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndio washindi).

Sayyid Hashim Baharani katika tafsiri ya Baharani na Ghaayatul-Maraam, amepokea hadithi kutoka kwa Swaduqu kutoka kwa Abu Jarudu kutoka kwa Abu Jafari (a.s) anasema: Kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo (Hakika kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini), kundi la Mayahudi lilisilimu, miongoni mwao Abdullahi bun Salaam, Tha’labu bun Yamini bun Suriya, wakamfuata Mtume (s.a.w.w). wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika Mussa alimuusia Yusha’a bun Nuun, nani wasii wako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Nani kiongozi wetu baada yako? Ndio ikashuka aya hiyo (Hakika kiongozi wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini wanao simamisha swala na kutoa zaka wakiwa kwenye rukuu).

Mtume (s.a.w.w) akasema: Simameni. Wakasimama na kwenda msikitini, wakakuta kuna muombaji anatoka msikitini, Mtume (s.a.w.w) akamuuliza, Ewe muombaji kuna mtu amekupa kitu? Akasema, ndio. Nimepewa hii pete. Akamuuliza, nani amekupa? Amenipa yule mtu anayeswali. Akamuuliza, alikupa akiwa katika hali gani? Akasema, alikua amerukuu, Mtume (s.a.w.w) akasoma takbira na watu waliokua msikitini wakasoma takbira.

Mtume (s.a.w.w) akasema: Ali ndio kiongozi wenu baada yangu, wakasema: Tumeridhia Allah ndio Mola wetu na Muhammad Mtume wetu na Ali bun Abu Twalib kiongozi wetu. Mwenyezi Mungu akashusha aya isemayo: (Mwenye kumtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndio washindi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: