Markazi Dirasaat Afriqiyya imefanya hafla ya Ghadiir katika nchi ya Naijeria kwa kupongeza mabinti 100

Maoni katika picha
Markazi ya Dirasaat Afriqiyya chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya hafla ya Idul-Ghadiir kwenye mji wa Kaduna nchini Naijeria katika bara la Afrika.

Sayyid Muslim Aljabiri kiongozi wa idara ya Tabligh katika Markazi hiyo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Markazi imepanua maadhimisho ya Idul-Ghadiir mwaka huu, ndani na nje ya Iraq, kwenye nchi tofauti za Afrika, ikiwemo Naijeria, kutokana na umuhimu wa tukio hilo na kuhuisha utiifu kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s)”.

Hafla iliyofanywa katika mji wa Kaduna ilikua na vipengele tofauti, ikiwa ni Pamoja na kupandisha pendera iliyotoka kwenye malalo ya mtoto wa aliyepewa baiyya Abulfadhil Abbasi (a.s), sambamba na kupongeza mabinti (100) waliofikisha umri wa kuwajibikiwa kisheria”.

Akaendelea kusema: “Hafla ilikua na tukio la kugawa zawadi kwa mabindi walioshiriki kwenye hafla hiyo, pamoja na kuwaelewesha maana ya kuwajibikiwa kisheria na wajibu wao katika Dini, furaha ilienea pia kwa wazazi na walezi wa mabinti hao, wakawa na furaha mbili, furaha ya Idul-Ghadiir na furaha ya mabinti zao kufikisha umri wa kuwajibikiwa kisheria”.

Kumbuka kuwa Markazi Dirasaat Afriqiyya hutumia matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kufanya harakati mbalimbali, likiwemo tukio hili la kutawalishwa kiongozi wa waumini Ali (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: