Watumishi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wameanza kuweka utaratibu wa kisheria kwa mawakibu za uombolezaji na utoaji wa huduma siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam (Ashura) mkoani Karbala, kwa kushirikiana na viongozi wa idara za ulinzi na usalama.
Rais wa kitengo hicho Sayyid Aqiil Abdulhussein Alyaasiriy amesema: “Utaratibu huo unahusisha mawakibu za kuomboleza na za utoaji wa huduma, zitakazo shiriki kwenye maadhimisho ya siku kumi ambazo ni rasmi kwa mawakibu za Karbala, miongoni mwa utaratibu huo ni kutoa vitambulisho maalum kwa viongozi wa mawakibu, ukizingatia kuwa kitengo hicho kinajukumu la kuratibu na kusimamia shughuli za mawakibu”.
Akaongeza kuwa: “Uwekaji wa taratibu za usimamizi kisheria ni miongoni mwa mambo muhimu katika utendaji wa mawakibu, kwa lengo la kuboresha utendaji wa mawakibu sambamba na kushirikiana na idara zingine”.
Akafafanua kuwa: “kitengo kinamajukumu ya aina mbili, kwanza: uratibu, unahusisha kubaini sehemu za kutoa huduma sambamba na kusimamia matembezi ya mawakibu za kuomboleza zitakazo kuja Karbala ndani ya siku kumi, ratiba itatolewa hivi karibuni.
Pili: Ulinzi na usalama, nalo ni jukumu la idara za askari wa Karbala, majukumu hayo hutolewa sambamba na utoaji wa vibali kwa mawakibu hizo, hakuna maukibu yeyote inayoweza kutoa huduma bila kibali”.
Kumbuka kuwa kitengo cha maadhimisho ndio chenye jukumu la kuratibu utendaji wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya, na kutoa vitambulisho na vibali kwa kushirikiana na idara za ulinzi na usalama, taasisi za kijamii ambazo husaidia mawakibu na vikundi vya Husseiniyya wao ni wahisani tu, hawawajibiki kisheria kuratibu na kupangilia utendaji wa mawakibu.