Kituo cha turathi za kiislamu katika mji wa Mash-had chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya semina mbili kuhusu uhakiki wa nakala-kale.
Semina hizo zimepewa jina la Ghadiir na kiongozi wa wanatauhidi, zimepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi wa hauza na wadau mbalimbali.
Semina hizo zimepambwa na majaribio ya nadhariyya na vitendo, chini ya usimamizi wa mkufunzi Shekhe Qais Atwaar, baada ya kuwafafanulia misingi ya lazima katika kufanya uhakiki kwa muda wa siku kumi, kwa kutumia saa moja na nusu kila siku.
Semina hizo ni sehemu ya juhudi za kitengo cha maarifa za kuandaa kizazi cha wahakiki bobezi, watakaofanya kazi hiyo na kuibua turathi za kiislamu na kuzisambaza.
Tambua kuwa kituo cha turathi za kiislamu kinajukumu la kuhuisha turathi za kiislamu, pia kimeshatoa machapisho mbalimbali kuhusu turathi, kuna machapisho mengine yatatoka hivi karibuni, na kuzipamba maktaba za kiislamu.