Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya Ghadiir katika mji wa Mosul

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni na maelekezo ya kimaendeleo chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya kilichopo katika wilaya ya Sanjaari kaskazini magharibi ya mkoa wa Mosul, kimefanya hafla ya Idul-Ghadiir Aghar, iliyo hudhuruwa na kundi kubwa la watu wa Sanjaari.

Msimamizi mkuu wa kituo hicho Shekhe Haidari Aridhwi kutoka kitengo cha Dini ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha utamaduni na maelekezo ya kimaendeleo, inaendelea kuhuisha turathi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kwenye kila tukio, likiwemo tukio hili la kutimia Dini na kutimiza neema kwa waislamu na waumini, kwa kutawalishwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Hafala ilikua na sehemu mbili, ya wanaume na wanawake, ilikua na vipengele vingi vilivyo jaa shangwe na furaha”.

Akabainisha kuwa: “Miongoni mwa vipengele vyake ni utoaji wa mhadhara kuhusu tukio hilo, iliotolewa na mkuu wa kituo Sayyid Muhmud A’araji, ameongea kuhusu umuhimu wa siku hiyo na aya zilizo shuka kuhusu tukio hilo na hadithi tukufu, pamoja na umuhimu wa kuhuisha siku hii tukufu ya kutawalishwa Imamu Ali (a.s) na kuhuisha utiifu kwake, na kuahidi kushikamana na mwenendo wake (a.s)”.

Akamaliza kwa kusema: “Hafla ilikua pia na vipengele vingine vilivyo onyesha furaha waliyokua nayo washiriki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: