Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa hafla ya kuhitimu wanafunzi elfu 8 walioshiriki kwenye mradi wa semina za Qur’ani za majira ya joto, iliyo hudhuriwa na viongozi wa Dini na sekula.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na mmoja wa wanafunzi wa mradi Abdullahi Raaidu, ikafuatiwa na surat Fatha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq.
ukafuata ujumbe kutoka kwa muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Shekhe Twariq Bagdad, amesifu kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya kupitia miradi mbalimbali ya utoaji wa huduma, bila kusahau mradi huu mtukufu, akamshukuru kila aliyesaidia kufanikiwa mradi huu wa Qur’ani tukufu.
Kisha ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulio wasilishwa na muwakilishi wa Ataba na rais wa Majmaa ya Qur’an Dokta Mushtaq Ali, amekaribisha washiriki na kupongeza juhudi za watendaji, akasisitiza kuwa: “Majmaa inapambana kurekebisha tabia za vijana na kuwalinda na mazingira mabaya yanayoweza kuharibu maadili yao ndio tukaamua kuweka semina hizi kwa ajili hiyo”.
Halafu wanafunzi wakaimba kaswida maalum inayohusu semina za Qur’ani za majira ya joto, likafuata shairi lililosomwa na mwanafunzi Hussein Alawi, na shairi lingine likasomwa na mwanafunzi Muhammad Baaqir Abbasi.
Hafla ikahitimishwa kwa kusoma kiapo cha utii kwa Imamu wa zama (a.f) kilicho ongozwa na mkuu wa Maahadi Shekhe Jawadi Nasrawi.