Kujadili njia ya ushirikiano.. ugeni kutoka chama cha mpira wa miguu cha Iraq umetembelea hospitali ya rufaa Alkafeel

Maoni katika picha
Ugeni kutoka chama cha miguu cha Iraq/ tawi la Karbala, umetembelea hospitali ya rufaa Alkafeel na kujadili njia za ushirikiano kati ya hospitali na chama hicho kuhusu matibabu ya wachezaji wa mpira.

Mkuu wa hospitali ya rufaa Alkafeel Dokta Jasim Ibrahimi amesema “Hospitali inaratiba ya kusaidia vijana wanaoshiriki michezo mbalimbali hapa Iraq, inauzowefu mkubwa wa kutibu watu wanaoumia michezoni kutoka mikoa tofauti na kuwawezesha kurudi tena uwanjani”.

Rais wa ugeni huo Abdurazaq Akram Shalaa amesema: “Tumeangalia huduma zinazotolewa na hospitali, kutakua na ushirikiano katika swala la matibabu ya wanamichezo wa Iraq”.

Akasisitiza kuwa: “Itapangwa siku maalum ya kufanyiwa vipimo wanamichezo walioumia au wagonjwa, uongozi wa hospitali uko tayali kusaidia wanamichezo wanaohitaji msada”.

Ugeni huo umesema kuwa: “Hospitali ya Alkafeel ni taasisi ya kitaifa yenye msaada mkubwa kwa wananchi, imepunguza gharama za matibabu ukilinganisha na hospitali sawa na hii zilizopo nje ya Iraq, tunajifakharisha kwa taasisi hii yapekee hapa Iraq, tutakuja kutembelea vitengo vya hospitali tukiwa pamoja na vyama vingine vya michezo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: