Muthanna imehitimisha mradi wa semina za majira ya joto kwa ushiriki wa wanafunzi 1500

Maoni katika picha
Mkoa wa Muthanna umehitimisha mradi wa semina za majira ya joto, unao endeshwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ushiriki wa wanafunzi 1500, wamesomeshwa Qur’ani tukufu, Aqida, Fiqhi, Akhlaq na Sira.

Hafla ilikua na vipengele vingi, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na mmoja wa wanafunzi wa mradi Mauhubu Hussein Haitham, ikafuata surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukasomwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa), halafu ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya uliotolewa na mkuu wa Maahadi ya Qur’ani Shekhe Jawadi Nasrawi, amewakaribisha washiriki na kupongeza juhudi za wasimamizi wa mradi hapa mkoani, kisha akasema sababu kuu ya mradi na kuusambaza mikoani, ni kujenga uwelewa wa Qur’ani tukufu na mafundisho ya Ahlulbait (a.s) kwa vijana, sambamba na kuwalinda na fikra potovu, akatangaza kufunguliwa kwa tawi la Maahadi katika mji wa Muthanna, na kuingia rasmi kwenye orodha ya matawi ya Maahadi ya mikoani.

Zikafuata kaswida maalum zilizo imbwa na wanafunzi wa mradi, kisha akapewa nafasi muimbaji Hussein Muswarii, halafu wakapewa zawadi watoto wa mashahidi walioshiriki kwenye mradi, mwisho kikasomwa kiapo cha utii kwa Imamu wa zama (a.f) kilicho ongozwa na msimamizi mkuu wa semina katika mkoa wa Muthanna Sayyid Muhammad Mussawi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: