Matarajio ya siku ya kwanza Muharam kwa mujibu wa ofisi ya Sayyid Sistani

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani katika mji wa Najafu, kwa mujibu wa jaduali la nyakati za miandamo, mwezi wa Muharam wa mwaka (1444h) kwenye mtandao wake rasmi, unaonyesha kuwa: Mwezi wa Muharam utaandama jioni ya siku ya Ijumaa (mwezi 29 Dhulhijja 1443h) sawa na tarehe (29 Julai 2022m), katika anga la mji wa Najafu wakati wa kuzama jua saa (07:02) kwa urefu wa daraja 8 na dakika 53, baada ya kuzama jua utabaki kwa muda wa dakika 46, kiwango cha mng’ao kitakua %0.77, unatarajiwa kuonekana kwa macho halisi iwapo anga likiwa safi bila mawingu.

Tambua kuwa: “Maelezo haya hayawakilishi rai ya Marjaa Dini mkuu, yametokana na matarajio ya wana-anga, kwa sababu mwanzo wa mwezi hutegemea kuthibiti kwa mwezi muandamo kisheria, tunawaomba waislamu wote waangalie mwezi kwa kufuata maelezo hayo, na kama wakiuona watupe taarifa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: