Kwa kuhudhuria kiongozi mkuu wa kisheria: Atabatu Abbasiyya imetoa zawadi kwa wanafunzi wa shule zake waliofaulu

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya kongamano la pili la kuzawadia wanafunzi waliopata nafasi za kwanza kwenye mitihani ya kuhitimi elimu ya msingi katika shule za Al-Ameed, alasiri ya leo siku ya Alkhamisi.

Utoaji huu wa zawadi ni muendelezo wa utoaji wa zawadi uliofanywa jana ndani ya ukumbi wa chuo kikuu cha Al-Ameed, na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na viongozi wengine, bila kusahau viongozi wa kamati ya malezi na elimu ya juu na wazazi wa wanafunzi hao.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Ibaa).

Ukafuata ujumbe kutoka kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, ulio wasilishwa na makamo kiongozi mkuu wa taaluma Dokta Haidari Al-A’raji, akahimiza umuhimu wa kusoma katika kutengeneza vizazi, akapongeza kazi nzuri inayofanywa na watumishi wa kitengo cha malezi na elimu, kufaulu kuzuri kwa wanafunzi kunatokana na juhudi zao, aidha akawashukuru wanafunzi na wazazi wao.

Mwisho wa hafla walimu waliofanya kazi kubwa ya ulezi na ufundishaji bora uliopelekea wanafunzi wao kufaulu kwa kiwango cha juu, wakapewa zawadi, pamoja na kugawa zawadi kwa wanafunzi walioshika nafasi za kwanza, sambamba na kuwahimiza kuendeleza juhudi hizo katika safari yao ya masomo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: