Ifahamu bendera.. maelezo kuhusu bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) itakayobandishwa usiku wa kwanza wa mwezi wa Muharam

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu usiku wa kwanza wa Muharam katika kila mwaka, hufanya ratiba maalum ya uombolezaji kwa kubadilisha bendera ya kubba tukufu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutoka bendera nyekundu na kuweka bendera nyeusi.

Bendera hiyo inaumaalum wake tofauti na bendera nyekundu ambayo hupeperushwa miezi kumi.

Kiongozi wa idara ya ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri Sayyid Abduzaharah Daud Salman amesema: “Watumishi wa idara yetu wamepata utukufu wa kushona bendera maalum itakayo peperushwa kwa muda wa miezi miwili Muharam na Safar, yenye randi nyeusi, imeshonywa kwa kitambaa cha kifahari na bora zaidi”.

Akaongeza kuwa: “Uzito wa bendera hiyo ni (kilo 2.5) takriban, vipimo vyake ni mita (3.5) upana, mita (2.5) urefu, inamaandishi pande mbili”.

Akaendelea kusema: “Kila upande wa bendera hiyo kumeandikwa maneno yasemayo ewe mnyweshaji wenyekiu Karbala (Yaa saaqi atwasha Karbala) kwa rangi nyekundu, neno hilo linahusu miezi miwili Muharam na Safar, yameandikwa kwa hati ya Thuluth, yanaukubwa wa mita (1.2) na sentimita ishirini, jumla yanachukua sehemu ya mita mbili na nusu (2.5) kwenye bendera yote”.

Akamaliza kwa kusema: “Ushonaji wa bendera hupitia hatua mbalimbali, kwanza ni kuchagua aina bora ya kitambaa, chenye uwezo wa kuvumilia mabadiliko ya hali ya hewa na kisicho pauka, kisha huchukuliwa vipimo maalum, halafu huanza kazi ya ushonaji, kuna sehemu hushonywa kwa mikono na zingine kwa mashine”.

Kumbuka kuwa bendera ya kubba tukufu -sawa hii inayopandishwa kwa miezi miwili Muharam na Safar au ile inayopandishwa katika miezi mingine ya mwaka-, hubadilishwa kila baada ya siku kumi, hivyo hutumika bendera tatu kila mwezi, hii ni kutokana na mazingira ya hali ya hewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: