Markazi dirasaat Afriqiyyah imesema: tutahuisha maombolezo ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) katika nchi 13 za Afrika

Maoni katika picha
Markazi dirasaati Afriqiyyah chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa, imeweka utaratibu wa kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein, familia yake na wafuasi wake (a.s) kwenye nchi 13 za Afrika.

Mkuu wa kituo hicho Shekhe Saadi Sataar Shimri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Markazi imeweka mkakati wa kuhuisha kumbukumbu ya Ashura katika nchi za (Senego, Gana, Tanzania, Brukinafaso, Siralion, Mali, Naijeria, Madagaska, Mauritania, Kamerun, Naija, Benin na Averkosti), zitafanyika majlisi za kuomboleza na harakati zingine ikiwa ni pamoja na vikao vya usomaji wa Qur’ani”.

Akaongeza kuwa: “Markazi hufanya majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Hussein katika nchi za Afrika kila mwaka, lakini mwaka huu tumeongeza idadi ya nchi na miji, jambo hilo limetokana na maelekezo ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akahitimisha kwa kusema: “Majlisi na harakati za uombolezaji zitafanyika kwa kipindi cha miezi miwili Muharam na Safar, watu wengi watanufaika na majlisi hizo, kauli mbiu inasema kukumbuka masaibu ya Imamu Hussein (a.s) ni kuhuisha uislamu asili uliofundishwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuhuisha amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: