Kuanza kwa shindano la Aljuud kwa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu

Maoni katika picha
Asubuhi ya Ijumaa ratiba ya shindano la Aljuud inayosimamiwa na idara ya tahfiidh chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Majmaa ya Qur’ani chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inayo husu wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu katika mji wa Karbala na mikoani, kwa ushiriki wa zaidi ya mahafidhu 50 walio hifadhi mazuju tofauti katika kitabu kitakatifu.

Shindano limefanyika ndani ya jengo la Alqami, ambapo wameshiriki wanafunzi wa Maahadi na matawi yake ya mikoani, chini ya kamati ya wataalamu inayoundwa na (Haafidh wa Qur’ani nzima Ustadh Ali Almayahi, anayeangalia ubora wa hifdhu, na Ustadh Nabiil Asadi anaeangalia kuanza na kusimama).

Mahafidhu walio shiriki wapo waliohifadhi juzuu 3, juzuu 5, juzuu 10, juzuu 15, juzuu 20, kulikua na ushindani mkubwa baina ya washiriki. Shindano hili linasaidia kuangalia vipaji vyao na kuwaandaa kwa ajili ya mashindano mengine ya kitaifa na kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: