Kukamilika kwa maandalizi ya kubadilisha bendera ya kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kukamilika kwa maandalizi ya kubadilisha bendera nyekundu inayopepea juu ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuweka bendera nyeusi ya huzuni na majonzi ya Husseiniyya, shughuli ya kubadilisha bendera itafanywa leo siku ya Ijumaa jioni.

Imeandaliwa sehemu maalum kwa ajili ya kazi hiyo, nayo ni uwanja wa katikati unaoelekea kwenye mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), maandalizi yote ya upandishaji wa bendera yamekamilika, aidha imeandaliwa sehemu ambayo itapandishwa bendera nyeusi ya kawaida inayo ashiria kubadilishwa kwa bendera ya kubba takatifu.

Imeandaliwa ratiba maalum ya shughuli hiyo itakayo fanywa baada ya kukamilika kwa upandishaji wa pendera kwenye kubba la Imamu Hussein (a.s), itahusisha usomaji wa Qur’ani na ujumbe kutoka kwenye uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kutakua na kaswida na mashairi ya kuomboleza, sambamba na kukabidhi bendera ya uombolezaji kwa moja ya mikoa ya Iraq, kutakua na upandishaji wa bendera nyeusi sehemu zilipo bendera nyekundu penbeni ya jukwaa.

Ratiba hiyo itakamilishwa kwa kupandisha bendera nyeusi juu ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) na mwisho kabisa zitasomwa tenzi na kaswida za kuomboleza.

Kumbuka kuwa shughuli hii imekua ikifanyika tangu mwaka (2004m), nayo ni ishara ya kuanza kwa mwezi wa huzuni katika mji mtukufu wa Karbala makao makuu ya maadhimisho ya Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: