Mji wa Karbala umeshuhudia kundi kubwa la watu wanaokuja kushiriki kwenye ratiba ya kubadilisha bendera ya kubba la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), shughuli ambayo itafanywa jioni ya leo siku ya Ijumaa baada ya swala ya Magharibi na Ishaa, tukio hilo ndio tangazo la kuanza msimu wa huzuni za Husseiniyya, jambo hili limezoweleka kwa miaka mingi.
Watu wengi wamesimama mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), sehemu ya mbele ya mlango wa Kibla itakapo fanyika shughuli hiyo, na kukumbuka yaliyowatokea watu wa nyumba ya Mtume (a.s) miaka (1400) iliyopita.
Kundi hilo la watu linakumbuka yaliyotokea kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika mwezi huu, na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu kwa baraka za watu waliosimama mbele ya malalo hiyo takatifu akubali ibada zao na awawezeshe kufuata mwenendo wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kumbuka kuwa jambo hili limekua likifanywa tangu mwaka (2004m), nalo ni sawa na tangazo la kuingia mwezi wa huzuni katika mji mtukufu wa Karbala makao makuu ya maadhimisho ya Husseiniyya.