Kubadilisha bendera za kubba la haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuwekwa bendera za huzuni na majonzi

Maoni katika picha
Jioni ya Ijumaa baada ya swala ya Magharibi na Isha, imefanywa shughuli ya kubadilisha bendera ya kubba la haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), zimeshushwa bendera nyukundu na kupandishwa nyeusi, kama ishara ya kuingia kwa mwezi wa Muharam (1444h) na kuanza msimu wa huzuni na majonzi.

Kama kawaida shughuli ilianzia katika Atabatu Husseiniyya tukufu, imeshushwa bendera nyekundu juu ya kubba la malalo ya Imamu Hussein (a.s) na kupandishwa nyeusi mbele ya kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Shekhe Abdulmahadi Karbalai na rais wa wakfu Shia, wagendi mbalimbali waliowakilisha sekta tofauti huku watu wengi wakijitokeza kushiriki.

Baada ya hapo wakaelekea kwenye malalo ya mbeba bendera ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kufanya shughuli ya kubadilisha bendera ya malalo hiyo takatifu, kwenye uwanja wa katikati ya mlango wa Kibla, mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na baadhi ya viongozi wa kidini na kijamii, bila kusahau wawakilishi wa sekta mbalimbali na kundi kubwa la waombolezaji waliofurika kwenye uwanja huo mtakatifu.

Shughuli ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Haidari Jalukhani, ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, akasema: “Enyi ndugu zangu kila mwaka usomaji wetu wa tukio la Twafu huonekana mpwa, huwa tunanufaika kwa kupata baraka juu ya baraka…”

Likafuata tukio la kukabidhi bendera ya uombolezaji kwa mkoa wa Muthanna, iliyopokewa na kiongozi anayewakilisha mawakibu za mkoa huo bwana Saadi Abdali, kisha zikapazwa sauti zikisema (Labbaika yaa Abbasi), halafu ikashushwa bendera nyekungu kwenye kubba takatifu, kazi hiyo imefanywa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aali Dhiyaau-Dini, na kupandishwa bendera nyeusi ya huzuni za Ashura.

Baada ya hapo yakasomwa mashairi ya uombolezaji, kaswida na tenzi za Ashura na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Ali Swafaar Karbakai, ikafuata majlisi ya maatam iliyo ongozwa na muimbaji Maahir Sultani Karbalai na ndio ukawa mwisho wa shughuli hiyo.

Kumbuka kuwa shughuli hii imekua ikifanywa tangu mwaka (2004), kwayo hukamilika tangazo la kuanza mwezi wa huzuni katika mji mtukufu wa Karbala, makao makuu ya maadhimisho ya Husseiniyya, shughuli hii ilisimama miaka miwili iliyopita kwa sababu ya janga la maambukizi ya virusi vya Korona na kuheshimu maelekezo ya idara ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: