Watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya Atabatu Abbasiyya wameweka mazingira ya huzuni kwenye uwanja wa katikati ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kama sehemu ya kuonyesha kuanza kwa kumbukumbu za kuuwawa kwao (a.s).
Rais wa kitengo tajwa Sayyid Naafii Mussawi amesema: “Maandalizi ya kupokea mwezi wa Muharam yalianza mapema chini ya maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi imefanyika kama ilivyo pangwa, jambo la kwanza lilikua kuweka mazingira ya huzuni kwa kufunga bendera na vitambaa vyeusi vilivyo andikwa maneno yanayoashiria kuomboleza msiba huu mkubwa ulio waliza Malaika, Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s)”.
Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa mambo ambayo hufanywa, ni kuweka bendera kwa idadi ya miaka ya Umri wa Imamu Hussein (a.s), zenye ukubwa wa mita moja na nusu, zimeandikwa (Ewe Hussein) na zingine zimeandikwa (Ewe mwezi wa bani Hashim), Pamoja na vitambaa (70) vyeusi vyenye ukubwa wa (mita 5 na nusu) vyenye ujumbe tofauti, vitambaa vingine hufungwa kwenye nguzo za taa”.
Akamaliza kwa kuwema: “Uwanja wa katikati ya haram mbili umekuwa na muonekano mweusi, upo tayali kupokea waombolezaji na kuwaonyesha ukubwa wa msiba huu”.
Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili hufanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara kubwa.