Mita elfu 10 za zulia jekundu zimetandikwa kwenye ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wametandika zulia jekundu ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwenye eneo lenye ukubwa wa mita elfu (10).

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Qurashi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Miongoni mwa maandalizi na kazi tulizopewa kwenye kitengo chetu, ya kujiandaa kupokea mazuwaru na mawakibu za waombolezaji, moja ya kazi zetu ni kutandika zulia jekundu ndani ya ukumbi wa haram kila mwaka katika siku kama hizi”.

Akaongeza kuwa: “Kutokana na umaalum wa mwezi wa Muharam sambamba na kuweka mazingira ya huzuni, ndani ya malalo takatifu, mwanzoni mwa mwezi huu hutandikwa zulia jekundu ukumbi wote wa haram takatifu, pamoja na kurahisisha matembezi ya mawakibu za kuomboleza zinazoingia ndani ya malalo takatifu”.

Akabainisha kuwa: “Kazi hiyo hufanywa usiku wa manane, kutokana na kumpungua idadi ya mazuwaru muda huo, huanza kutandua mazulia yaliyokuwepo na kuyapeleka kwenye kituo cha kuosha mazulia kilicho chini ya Ataba tukufu, kisha kutandikwa nailoni halafu ndio tunatandika zulia juu yake”.

Akafafanua kuwa: “Tumetandika ndani ya ukumbi wa haram na milangoni, mazulia yametandikwa kwa kuunganishwa na kuyafanya linakua kama zulia moja”.

Kumbuka kuwa kitengo kinachosimamia ukumbi wa haram tukufu kinamajukumu mengi, na huongezeka zaidi wakati wa ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, kama ziara ya Ashura na Arubaini, ambapo husimamia matembezi ya mawakibu za kuomboleza na mazuwaru ili kuzuwia msongamano baina yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: