Ratiba ya (Ulizeni wanaojua) mwezi wa Muharam huwa na program mbalimbali za uombolezaji

Maoni katika picha
Ratiba ya (Ulizeni wanaojua) hufanywa kila wiki na idara ya Qur’ani, chini ya ofisi ya maelekezo ya kidini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, katika mwezi wa Muharam huwa kunavipengele vingi vya uombolezaji.

Kiongozi wa idara bibi Fatuma Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ratiba inayofanywa katika ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) -kwenye sardabu ya Imamu Alkadhim a.s-, ni endelevu na inalenga mazuwaru wa malalo hiyo takatifu, hususan katika mwezi wa huzuni mwezi wa Muharam kwa ajili ya kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) kutokana na kifo cha bwana wa mashahidi na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba huanza kwa kusoma juzuu moja la Qur’ani tukufu na kuelekeza thawabu zake kwa Imamu Hussein (a.s), baada ya hapo hufuata mhadhara elekezi wa mazuwaru watukufu, kuhusu namna ya kunufaika na siku hizi tukufu, na jinsi ya kufanyia kazi kwa vitendo harakati ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya majlisi za kuomboleza na kusoma dua ya Imamu wa zama (a.f)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: