Mawakibu za kuomboleza za Karbala zimeanza kufanya maombolezo ya kifo cha Imamu Hussein (a.s), asubuhi ya leo siku ya Jumapili, siku ya kwanza katika mwezi mtukufu wa Muharam, msimu wa maombolezo umeanza rasmi.
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Aqiil Abdul-Hussein Alyasiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shughuli za uombolezaji ambazo hufanywa siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam na watu wa Karbala, ni desturi ya toka zamani kuwa na maukibu za uombolezaji na (Zanjiil)”.
Akabainisha kuwa: “Mawakibu za uombolezaji hutembea katika barabara maalum zinazo elekea kwenye mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi kwenye ukumbi wa haram tukufu, kisha hutokea mlango wa Imamu Hassan (a.s) na kuelekea kwenye malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Abu Abdillahi Hussein (a.s), kwa kupita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu”.
Akafafanua kuwa: “Tumeandaa kamati maalum ya watumishi wa kitengo chetu inayotembea pamoja na mawakibu kuanzia mwanzo hadi mwisho, inajukumu la kusimamia matembezi na kuhakikisha hautokea msongamano wowote wala matembezi hayo hayatatizi shughuli za mazuwaru wengine”.
Maukibu za zanjiil huundwa na kundi la watu waliovaa nguo nyeusi na kushika shada la minyororo midogomidogo, ambayo hujipiga nayo mabegani kwao kwa utaratibu maalum sambamba na mdundo wa ngoma, hutembea barabarani hadi kwenye malalo mbili takatifu huku wakiimba kaswida za huzuni (Yaa Hussein.. madhluumu Hussein shahidi atwishaan).
Siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam ni maalum kwa ajili ya mawakibu za watu wa Karbala za kuomboleza na kutoa huduma.