Usafi mkubwa unafanywa kwenye maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya usafi mfululizo kwenye maeneo yanayo zunguka haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kwenye njia zinazo elekea kwenye haram hiyo, kwa ajili ya kujiandaa kuupokea mwezi mtukufu wa Muharam na maombolezo ya Ashura.

Kiongozi wa idara ya usafi chini ya kitengo tajwa Sayyid Mustafa Hassan Haadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi ya usafi inayofanywa na watoa huduma wetu pamoja na wasaidizi wa kujitolea huongezeka katika siku kama hizi za kujiandaa na maombolezo ya Ashura”.

Akaongeza kuwa: “Tumeanza kazi ya kusafisha maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na vituo vya kutoa huduma zikiwemo sehemu za kutunza amana za watu, kuweka viatu, sambamba na barabara zinazo elekea haram tukufu, hali kadhalika sehemu zote za bustani, sehemu za maji ya kunywa na maeneo mengine, tunatumia kila aina ya zana na uwezo wote kwa ajili ya kuhakikisha mazingira yanakua safi”.

Tambua kuwa idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa idara muhimu katika kuhakikisha Atabatu Abbasiyya na maeneo yanyoizunguka yanakua safi wakati wote.

Kumbuka kuwa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa vitengo ambavyo hutoa huduma ya moja kwa moja kwa mazuwaru, hufanya kila kiwezalo kuhakikisha kinatoa huduma bora zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: