Kuwasiri Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala mwezi pili Muharam

Maoni katika picha
Riwaya zinaonyesha kuwa mwezi pili Muharam mwaka wa sitini na moja hijiriyya, msafara wa Imamu Hussein (a.s) uliwasiri katika ardhi ya Karbala, na ilikua siku ya Alkhamisi.

Imamu Hussein (a.s) alionyesha kuitambua ardhi hiyo, pale aliposema: “Tushuke hapa, hapa ni kituo cha msafara wetu, hapa zitamwagwa damu zetu, hapa tutavunjiwa heshima zetu, hapa watauliwa watu wetu, hapa watachinjwa watoto wetu, hapa yatatembelewa makaburi yetu, ardhi hii aliniahidi babu yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), akashuka kwenye farasi wake, likajengwa hema lake na mahema ya watu wa familia yake, kisha yakajengwa mahema ya wafuasi wake”.

Huru bun Yazidi akaweka kambi karibu na Imamu Hussein (a.s) akiwa na wapanda farasi elfu moja, akaandika barua kwa Ubaidullahi bun Ziyadi ya kumjulisha kuwa Imamu Hussein yupo katika ardhi ya Karbala.

Ilipofika kesho yake akaja Omari bun Saadi bun Waqaas kutoka katika mji wa Kufa akiwa na wapanda farasi elfu 4000, wakaunganda na wabanda farasi elfu moja wa Huru bun Yazidi Ariyahi, wakawa jumla askari wapanda farasi elfu tano, Ibun Ziyadi akaendelea kutuma askari hadi wakafika elfu thelathini wapanda farasi na watembea kwa miguu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: