Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kutekeleza hatua ya kwanza ya mkakati maalum wa mwezi wa Muharam

Maoni katika picha
Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kutekeleza hatua ya kwanza, ya mkakati wa ulinzi na utoaji wa huduma katika kuhuisha kumbukumbu ya Ashura, walianza toka siku ya hafla ya kubadilisha bendera ya kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s), hafla iliyohudhuriwa na watu wengi na wataendelea hadi siku ya kumi ya mwezi mtukufu wa Muharam.

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mkakati uliowekwa na Atabatu Abbasiyya ni utangulizi wa mkakati mkubwa utakaotekelezwa kwenye ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), Ataba imekamilisha maandalizi yote yanayo hitajika kwa mazuwaru na mawakibu Husseiniyya”.

Akaongeza kuwa: “Sehemu ya mkakati huo inatekelezwa kwa kushirikiana na Atabatu Husseiniyya pamoja na idara za ulinzi na usalama za hapa mkoani, na sehemu inatekelezwa na Atabatu Abbasiyya kupitia vitengo vyake, utekelezaji unafanywa kwa awamu kulingana na mahitaji, unaongezeka kidogokidogo hadi siku ya Ashura na kuhitimisha katika matembezi ya Towareji, na mengineyo miongoni mwa mambo ya uombolezaji”.

Kumbuka kuwa vitengo vyote vya Ataba tukufu vilitangaza kuwa vimekamilisha maandalizi ya ziara, vitahakikisha inakua ziara tulivu isiyokua na msongamano unaotatiza mazuwaru katika uingiaji na utokaji wa mawakibu za waombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: