Siku zote kumi za Ashura.. sajili jina lako kwenye ratiba kubwa ya Ashura kwa niaba kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Idara ya teknolojia na taaluma za mitandao chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya imetangaza ratiba kubwa ya kiibada na uombolezaji katika siku kumi za kwanza za mwezi wa Muharam, kupitia App inayopatikana kwenye simu za kisasa (smartphone) ziara kwa niaba, ukurasa maalum uliopo kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel, mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kiongozi wa idara tajwa Sayyid Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema: “Huduma hiyo hutolewa na mtandao kwa kila mpenzi wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao, huratibiwa kwa kushirikiana na idara ya masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya ambao hufanya ibada hizo”.

Akaongeza kuwa: “Mambo makubwa yanayofanywa katika ratiba hii ya kuomboleza msiba wa bwana wa mashahidi na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake (a.s) ni:

  • - Kufanya ziara kila siku ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Swala ya rakaa mbili mbele ya malalo mbili takatifu kwa kila aliyejisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba.
  • - Kusoma ziara ya Ashura kila siku ndani ya malalo mbili takatifu.
  • - Kutaja majina ya watu wote waliojisajili kwenye dua ya kumaliza majlisi za kuomboleza zinazofanywa katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Kufanya baadhi ya ibada na nyeradi maalum zinazohusiana na siku hizi kwa niaba.
  • - Kilele cha ratiba hiyo ni ziara maalum ya Ashura itakayo fanywa muharam kumi ndani ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na swala ya rakaa mbili ya ziara.

Tambua kuwa usajili unafanyika kupitia link ya ziara kwa niaba au App ya Atabatu Abbasiyya tukufu inayopatikana kwenye simu za kisasa (smartphone).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: